Meja Jenerali Francis Ogolla amechukua usukani rasmi hii leo kama mkuu wa vikosi vya jeshi vya kenya, KDF. Meja Jenerali Ogolla amechukua nafasi ya meja jenerali mstaafu robert kibochi aliyehudumu kwa miaka mitatu. katika uga wa michezo wa ulinzi complex eneo la langata jijini nairobi meja jenerali mstaafu Robert Kibochi aliandaliwa hafla ya heshima ya kwaheri. akimkabidhi mamlaka mkuu mpya wa KDF, meja jenerali mstaafu amesema uongozi wake utakumbukwa kwa ujasiri na maendeleo mengi.
Ещё видео!