Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani ya Chadema, Boniface Jacob ‘Boni Yai’ amesema Watanzania watarajie kushangazwa na mgombea urais atakayesimamishwa na chama hicho, kwenye uchaguzi mkuu wa 2025, kwani historia inaonyesha hivyo.
Boni Yai alibainisha hayo kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika hivi karibuni ambapo amezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo ikiwemo mbio za urais ndani ya chama chake kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.
Mwanasiasa huyo machachari alieleza hayo baada ya kuulizwa kuhusu mtu anayefaa kuwania urais kupitia chama hicho, akisema: “sina uhakika sana, kwa muda wangu wa miaka 19 niliokaa ndani ya Chadema, ni chama chenye ‘surprise’ (kushangaza) kuhusu mgombea urais.”
“Chadema haitabiriki tunaweza tukaenda katika uchaguzi mkuu wa mwaka ukaambiwa Kikwete (Jakaya, Rais mstaafu wa awamu ya nne) au Mizengo Pinda (waziri mkuu mstaafu) wagombea urais ukashangaa na inawezekana,” alisema Boni Yai.
Soma kwa undani kupitia www.mwananchi.co.tz
Ещё видео!