Wafanyabiashara wanne na wakazi wa jiji hili wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin kilo 30.
Washtakiwa hao ni Said Mbasha(24) mkazi wa Kinondoni; Joseph Dalidali(27) maarufu Kama Mbezi Tangibovu; Allu Murugwa( 24) mkazi wa Kijitonyama na Fatima Shomari(24).
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao, leo, Machi 11, 2021 na wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya.
Haya hivyo, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilikana na Hakimu Isaya ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 24, 2021 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
Ещё видео!