Available on all Platforms: [ Ссылка ]
Download or listen online: [ Ссылка ]
Performers: St. Benedict Catholic Choir, Rapogi
Producer: Verony Productions Ltd.
Composer: Ochien'g Odongo
Copyright ©Verony Productions Ltd.
Nikikumbuka pendo lako ee Yesu wangu (kweli) machozi ya furaha yananitoka. Jinsi ulivyo nifilia msalabani (kweli) nafsi yangu ipate kukombolewa.
Wewe Bwana nguvu zangu nijalie pendo lako niwapende ndugu zangu kama nafsi yangu x2
Pendo la Bwana Yesu ni pendo la ajabu (kweli) ni pendo la agape pendo la Mungu. Kajitolea kwetu bila hata malipo (Bwana) kafa msalabani kwa ajili yetu.
Tazama jinsi ilivyo vyema na tena vizuri (sana) ndugu kuishi pamoja kwa amani. Tuwapende wenzetu kama tunavyojipenda (sisi) vile Mungu mwenyewe anatupenda.
Tumesikia torati ya kale inavyosema (kwamba) mpende jirani yako akupendaye. Walakini umchukie adui yako kweli (kweli). Kwani ni jicho kwa jicho jino kwa jino.
Tumepewa amri kuu ya upendo wa Mungu (Baba) tuwapende wenzetu kwa moyo wote. Tuwapendeni adui zetu na kuwaombea (sana) waishi kuziona Baraka za Mungu.
Ещё видео!