Timu ya Simba SC imewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo, Desemba 10, 2024, ikitokea Algeria ilipokwenda kucheza dhidi ya CS Constantine na kufungwa 2-1 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Baada ya kurejea, sasa Simba inajiandaa kwa ajili ya mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya michuano hiyo dhidi ya CS Sfaxien kutoka Tunisia uliopangwa kuchezwa Desemba 15, 2024, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Nahodha wa Simba SC, Mohamed Hussein 'Tshabalala', amesema licha ya kupoteza mechi ya ugenini, lakini hawajakata tamaa. Amebainisha kuwa nguvu zote sasa zinalenga mechi za nyumbani, huku akiwapongeza CS Sfaxien kama timu yenye ubora.
Tshabalala ameongeza kuwa wachezaji wa Simba wanajipanga kwa bidii kuhakikisha wanavuna pointi tatu katika mchezo huo ujao.
#samiasuluhuhassan #simbasc #yangasc #mashabiki #nbcpremeireleague #cafchampionsleague #cafconfiderationcup #ikulumawasiliano #entertainment #music #news #yangasc #simbasc #cafchampionsleague #mayele #highlights #cafconfiderationcup #riversunited #mashabiki #yangaleo #yanga #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko #entertainment #music #news #magoliyasimba #magoliyayanga #magoliyote #magoliyamayele #mayele #aziziki #manara #manaraleo #ikulumawasiliano #magufuli #kikwete #mayele #singidabigstars #magoliyamayele #magoliyasimba #magoliyayanga #highlights #azamsportsfederationcup #chama #Shot #mamelodisundowns #alahlytv #alahlysc #miraj
Ещё видео!