Ni wimbo kutoka kitabu cha Tenzi za Rohoni, ambao umeimbwa na timu yetu ya CCC kutukumbusha kuwa hapa duniani tunapita tu. Tunahitaji kuongozwa na Bwana Mungu kwa kila jambo tunalolifanya.
Je wewe unamwomba nani akuongoze. Yesu kristo alishinda kifo kwa nguvu zote. Basi hatutaanza kumsifu.
1. Niongoze, Bwana Mungu, Ni msafiri chini;
Ni mnyonge, nguvu Sina; Nishike mkononi,
U mkate wa Mbinguni, (Nilishe siku zote) x2
2. Kijito cha maji mema Kitokacho mwambani,
Nguzo yako, moto,wingu Yaongoza jangwani
Niokoe Mwenye nguvu (Nguvu zangu na ngao) x2
3 . Nikikaribia kufa Sichi neno lo lote
Wewe kifo umeshinda Zinawe nguvu zote.
Tutaimba sifa zako,(Kwako juu milele) x2.
Tutaimba sifa zako,(Kwako juu milele) x2.
Ещё видео!