WATU 42 WAFARIKI BAADA YA KUNYWA POMBE YENYE SUMU, 100 WAPO KWENYE HALI MBAYA, SERIKALI YATOA TAMKO
Watu 42 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 100 wamenusurika kifo baada ya kunywa pombe yenye sumu nchini India.
Ripoti inaeleza kuwa watu hao walionusurika kifo hali zao ni mbaya hivyo wamepelekwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Taarifa hiyo imethibitishwa na Polisi nchini India na kueleza kwamba mamia ya watu waliaanza kuuguwa mapema wiki hii baada ya kunywa pombe inayokisiwa kuwa na kemikali ya Methanol.
Taarifa inaeleza kwamba tukio hilo limetokea katika Wilaya ya Gujarat huku mamlaka ya eneo hilo ikieleza kwamba operesheni ya uchunguzi wa pombe hiyo tayari imeanza.
Aidha, Polisi wamesema watu 31 wamefariki katika Wilaya ya Botad baada ya kuathirika na pombe hiyo huku wengine 11 wakifariki katika wilaya nyengine ya Ahmedabad iliyopo jirani na Wilaya ya Botad.
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ametoa tamko kuwa pombe hiyo hairuhusiwi kuuzwa nchini humo hususani katika Jimbo la Gujarat.
Mamlaka ya jimbo hilo tayari imeanza operesheni maalum katika baadhi ya maduka yanayouza vinywaji vya pombe kisha kukamata wahudumu.
Taarifa inaeleza kuwa mamia ya raia huripotiwa kufariki nchini India kila mwaka kutokana na unywaji wa pombe ya bei ya chini inayotengenezwa bila ya kuzingatia vigezo.
Kati ya lita bilioni tano ya pombe inayonyweka nchini India, asilimia 40 huwa imetengenzwa bila kuzingatia kanuni na usalama wa kutengeneza bidhaa hiyo.
Pombe hiyo hutia kemikali ya methanol kama njia ya kuongeza makali yake na iwapo itatumika na binadamu kwa mara nyingi husababisha upofu, kuharibika kwa figo au hata kifo.
Ripoti inaeleza kuwa mwaka 2021, watu 98 walifariki Kaskazini mwa Mkoa wa Punjab baada ya kunywa pombe hatari huku mwaka 2019 zaidi ya watu 150 waliripotiwa kufariki Kaskazini Mashariki mwa Jimbo la Assam baada ya kunywa pombe mbaya.
⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: [ Ссылка ]
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:[ Ссылка ]
⚫️ iOS:[ Ссылка ]
⚫️ VISIT COMEDY PLAYLIST: [ Ссылка ]
⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 657 693 210), ( +255 784 888982)
⚫️ Email: globaltvonlinenews@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com
⚫️ OUR PLAYLISTS:
⚫️ MICHEZO na BURUDANI: [ Ссылка ]
⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: [ Ссылка ]
⚫️ GLOBAL RADIO TV: [ Ссылка ]
⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: [ Ссылка ]
⚫️ Subscribe Global TV [ Ссылка ]
Ещё видео!