Katibu katika wizara ya usalama wa taifa, Raymond Omollo amesema maafisa kadhaa wa polisi ni miongoni mwa Wakenya milioni-4.7 waliotekwa na uraibu wa mihadarati. Omollo alisema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa dhidi ya ulanguzi na utumizi wa mihadarati. Serikali inatarajiwa kubuni vituo vya kuwarekebisha waraibu wa mihadarati humu nchini. Shirika la kukabiliana na uraibu wa pombe na mihadarati-NACADA limekariri kuwa watumiaji mihadarati wanapaswa kurekebishwa na sio kukamatwa kwani hilo ni tatizo la kiafya.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channell: [ Ссылка ]
Follow us on Twitter: [ Ссылка ]
Find us on Facebook: [ Ссылка ]
Check our website: [ Ссылка ]
#kbcchannel1 #drugabuse
Ещё видео!