SERIKALI YAANZA KUFANYA MABORESHO YA BARABARA MAKETE
Wakati msimu wa Mvua ukielekea mwisho, @tanroadshq wameanza ukarabati wa Barabara mbalimbali kuzunguka Wilaya ya Makete
Hapa ni Ukarabati wa Barabara ya Kitulo-Mpangala-Matamba
Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amekutana na Wenyeviti wa Vitongoji na Serikali za Vijiji Kata ya Kinyika kuzungumza masuala mbalimbali ya Kimaendeleo ikiwemo utekelezaji wa miradi ya Barabara, Elimu, Afya n.k
Mhe. Sweda amepokea changamoto ya Barabara ya Kinyika, Mwambwalo-Kikondo ambapo kwa sasa Barabara hiyo imefunga haipitiki na kuwaagiza TARURA kuleta mitambo haraka iwezekanavyo kufanya ukarabati wa miundombinu hiyo aambayo Serikali ilishatenga fedha.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwambwalo Kijiji cha Kinyika Aloyce Sanga amesema uchumi wa Wananchi wa Kitongoji hicho na Bonde la Matamba umeporomoka kwa sababu ya ubovu wa Barabara kwa kuwa wananchi wa Kata ya Kinyika, Matamba na maeneo jirani wengi wao wanajishughulisha na Kilimo cha Viazi.
Ещё видео!