Profesa Shivji: Dira ya Taifa Haina Muda Maalum.Tusikubali Kufanyiwa Majaribio
Akizungumza leo Juni 08,2024, katika kongamano la kwanza la kitaifa la maandalizi ya dira ya taifa ya maendeleo lililofanyika katika ukumbi wa Nkurumah, Profesa Issa Shivji ameeleza kuwa dira ya taifa ni tofauti na mipango ya maendeleo yenye muda maalum.
"Dira haina maana ya mpango wa maendeleo, mpango wa maendeleo unakuwa wa muda maalum. Kwa maoni yangu dira haina muda maalum," ameeleza Profesa Shivji.
Profesa Shivji alifafanua Zaidi kuwa moja ya mfano wa dira ya taifa ni Azimio la Arusha. Akijibu hoja hii Waziri wa OR Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo alieleza kuwa wameyapokea maoni hayo.
Katika wasilisho lake hilo Shivji ameasa juu ya taifa kuepuka kufanyiwa majaribio katika utengenezaji wa dira yake.
"Tusikubali kufanyiwa majaribio, majaribio yaliyofanyika miaka ya 1960 yanatosha. Tuwashirikishe wananchi kikamilifu popote pale walipo tupate maoni yao kuhusu nchi wanayotaka, Tanzania wanayoitamani, matamanio yao yapewe kipaumbele.Hii haiwezekani bila kuwa na mjadala wa kitaifa," alieleza Profesa Shivji.
Alifafanua Zaidi: "Tusifanye ile tuliyozoea wananchi wanatoa maoni, halafu wataalamu ndio wanachambua maoni haya. Popote pale walipo wananchi; vijijini, viwandani, mashuleni na kadhalika ili kujenga muafaka wa nchi tunayoitaka. Na mengine ya kupanga mpango wa muda mrefu wa muda mfupi itafuata."
Ещё видео!