Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel amesema Serikali imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 187 kwa ajili ya kujenga kiwanda cha chanjo za Covid 19, zitakazozalishwa hapa nchini.
Amesema pia Serikali imetenga Bilioni moja kwa ajili ya kununua magari ya wagonjwa 150 ambayo yatasambazwa nchini ambapo kati ya hayo Wilaya ya Chalinze itapatiwa gari moja.
Mollel pia amesema Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete aliomba milioni 418 na Serikali imeridhia kutoa fedha hizo kwa awamu kwa ajili ya umaliziaji wa majengo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze.
Ещё видео!