Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha miradi ya dharura iliyo chini yake.
Waziri Ulega ametoa maagizo hayo kwenye mkutano wake na menejimenti na mameneja wa TANROADS wa mikoa yote nchini uliofanyika mjini Dodoma, ambapo ameagiza miradi ya dharura inapaswa kushughulikiwa kidharura.
"Fanyeni kazi kwa kasi usiku na mchana hususan kwenye miradi ya dharura ili kuwawezesha Watanzania kuondokana na adha ya miundombinu iliyoharibiwa,” amesema Ulega.
Ulega amewaambia mameneja hao kuwa wanatakiwa kwenda kwa kasi inayofanana na viwango vya kasi vinavyoonekana wakati Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapopewa majukumu ya utekelezaji na Serikali kwa sababu kuna mvua zinakuja na zinaweza kufanya maeneo yaliyoharibika kuharibika zaidi.
Amesema barabara zilizoharibika kwa sababu ya mvua za masika zilizochanganyika na zile za El Niño zimesababisha usumbufu na kusimamisha shughuli za uchumi na hivyo, ni muhimu zikashughulikiwa kwa haraka.
Ещё видео!