Ni miaka minne tangu kutokea tukio lililoiacha familia ya bwana Nazari Sanga ikitangatanga baada ya Mpangaji wao kuuza nyumba walioyokuwa wakiishi Jijini Daresalaam katika mtaa wa Kunduchi Mtongani,
Kisa hiki kanamtuhumu Bwana costantino Siwale kwa kuuza nyumba ya Bwana Nazari Sanga ili kufidia kilo 38 za nyama zilizoharibika kwa madai ya kukatiwa umeme katika fremu aliyopanga na kusababisha kuharibika kwa nyama aliyokuwa anauza.
Shauri hili lilipelekwa katika Mahakama ya Mwanzo Kawe na ikaamuru kuuzwa kwa nyumba yenye thamani ya zaidi ya milioni 100 kwa kiasi cha shilingi milioni 8 huku mzee Sanga na Mtoto wake wa kiume aliyefahamika kwa jina la John Sanga wakiswekwa rumande kutumikia kifungo cha miezi mitano kwa kila mmoja,
Katika harakati za kuisaka haki yao iliyopotea familia hii imeweza kufika kwa Mbunge wa jimbo la kawe Mh. Askofu Josephat Gwajima ambaye amehuzunishwa sana na kisa hiki na kuahidi kuwasaidia.
Ещё видео!