Leo tunaanza kusoma kitabu cha Marko, na tunaenda kufanya maombi ya kufungua mbingu katika ulimwengu wa roho. Lengo la maombi ya siku ya leo ni kuondoa vikwazo na vizuizi vinavyozuia maombi na majibu ya maombi yetu.
Inawezekana ukafanya maombi na Mungu akakujibu, lakini majibu yako yakazuiliwa katika ulimwengu wa roho. Lakini pia inawezekana ukafanya maombi kwa imani, lakini maombi yako yakazuiliwa yasifike kwa Mungu.
Na siku ya leo tunaenda kuvunja huo upinzani, ili tuweze kuwa na ushindi katika maombi yetu. Kwa hiyo tutakapokuwa tunaomba, omba kwa imani, lakini pia tumia mamlaka uliyopewa na uhakikishe unapata ushindi.
Nami nakuombea ili YESU akufungue na akuondolee vizuizi vinavyosimama kinyume na maisha yako katika ulimwengu wa roho. Nakuombea kuanzia siku ya leo uanze kuona wepesi kwenye maombi yako na YESU akupe haja za moyo wako. Mungu akubariki sana na kukutunza daima. Amen
Isaac Javan | +255 745 76 545 72
Ещё видео!