Simba SC wametinga fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2020 kwa mikwaju ya penati 3-2 dhidi ya Azam FC baada ya dakika 90 kumalizika bila bao na kuivua rasmi ubingwa Azam FC.
Katika mechi hiyo ya nusu fainali iliyopigwa leo tarehe 10/01/2020 kwenye dimba la Amaan Zanzibar, Simba wamefunga penati zao kupitia kwa Erasto Nyoni, John Bocco na Jonas Mkude huku penati za Azam zikifungwa na Yakubu Mohamed na Bruce Kangwa.
Waliokosa penati upande wa Simba ni Sharaf Shiboub na Medie Kagere zote zikipanguliwa na golikipa Razak Abalora, kabla yay eye mwenyewe Abalora kukosa penati yake iliyodakwa na Beno Kakolanya. Wengine waliokosa ni Idd Kipagwile na Donald Ngoma.
Ещё видео!