Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, ameipa Serikali siku tano kutoa kauli ya Serikali Bungeni kuhusu hatua za dharura ambazo inazichukua ili kudhibiti ongezeko la bei ya mafuta nchini hali iliyosababisha kupanda kwa gharama za maisha.
Agizo hilo limetolewa leo Mei 5, 2022 Bungeni jijini Dodoma baada ya hoja ya dharura iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kilindi Mkoani Tanga, Omary Kigua ya kuliomba Bunge lijadili kwa dharula na kutafuta suluhu ya kuwapunguzia Wananchi ukali wa maisha unaosababishwa na ongezeko la bei ya mafuta.
Ещё видео!