Mwaka mmoja tangu watoto pacha Gracious na Precious waliokuwa wameungana maeneo tumboni na kwenye maini wafanyiwe upasuaji wa kutenganishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa mafanikio baada ya kuzaliwa wakiwa wameungana leo wamekabidhiwa nyumba ya kisasa ya kuishi.
Nyumba hiyo imejengwa na Benki ya UBA kwa gharama ya Sh. milioni 18, imekabidhiwa kwa wazazi wa watoto hao leo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwogelo.
Jokate amesema ujenzi wa nyumba hiyo umekamilika kwa siku 28, baada ya maandalizi ya muda mrefu ya kutafuta eneo lililopo karibu na huduma za kijamii kama shule na kituo cha afya kupatikana.
Aidha amesema eneo hilo lilinunuliwa na Balozi wa Visiwa vya Shelisheli Maryvonne Pool na benki ya UBA waligharamia ujenzi wa nyumba hiyo na kuweka umeme
Ещё видео!