MBOGO au Nyati ni mnyama jamii ya ng’ombe ambayo waishi msituni, porini (mapori ya wazi), mbugani, vichakani kwenye milima lakini hupendelea zaidi vichaka na matete mapana au manene. Rangi ya Nyati ni Kijivu iliyokoza.
Ni moja ya wanyama watano wakubwa katika wanyama wanaoishi nchi kavu (BIG FIVE ANIMALS).
Kuna aina mbili za mbogo, ambazo ni;
1. Nyati wa Afrika, Hafugiki.
Nyati wa msituni
Nyati wa savanna
2. Nyati maji, huyu hupatikana Bara la Asia na pia anaweza kufugwa.
Uzito wa Nyati wa Afrika (Nyati wa msituni) ni 265 – 320 Kg na Nyati wa savanna ni 500 – 900 Kg. Ni wakubwa kwa maumbo maana wanaurefu wa mita 1.7 hadi 3.4
Akiwa porini Nyati anaweza kuishi miaka 16 – 20, lakini akiwekwa kwenye zoo anaweza kuishi miaka 20 – 29.
Nyati huwa na pembe zilizojikunja mithili ya ndoano, dume huwa na pembe kubwa zaidi ya jike (Savanna), Nyati wa msituni pembe zao zimenyooka. Wanamasikio makubwa yaliyoyalala na husimama pale anapohisi hatari. Wanauwezo wa kukimbia wastani wa km 57 kwa saa na kutembea wastani wa km 5.4 kwa saa. Wanauwezo mkubwa wa kunusa na kutambua harufu mbalimbali. Lakini pia wanauwezo wa kusikia mbali sana, (nyati wa afrika).
Nyati ni mnyama anayekula nyasi ndefu kama ilivyo kwa Pundamilia hivyo husaidia wanyama wanaokula nyasi fupi kupata chakula bila shida.
Hutumia saa 18 kwa kula kwa siku huku wakitembea.
Katika maeneo ambayo yameathiriwa na shughuli za binadamu, Nyati hubadirisha ratiba yao ya kula na hivyo hula wakati wa usiku ambapo shughuli za binadamu zimesimama, hii ni kwa sababu hawataki usumbufu wakati wa kula.
Huwa wanakunywa maji kila siku hivyo hukaa karibu na vyanzo vya maji vya kudumu ili iwe rahisi kwao kupata maji ya kunywa pale wanapohitaji kunywa maji. Hunywa wakati wa Asubuhi.
Wakati wa kiangazi maji yanapokauka, hujikusanya eneo ambalo umbali wa kupata maji aridhini ni mfupi na hivyo huanza kuchimba kwa kupiga miguu yao chini hadi wanapoyapata maji.
Ещё видео!