Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Spika wa Bunge ameshaandikiwa barua na anajua kabisa wale wabunge 19 wa viti maalumu sio wabunge walioteuliwa na chama.
Mbowe amesema hayo leo Ijumaa Machi 18, 2022 jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi Machi 16.
Amesema Baraza Kuu litakaa mwezi ujao tarehe 24 na kama kuna rufaa zao tutaziona.
“Chadema haijawahi kuteua Kamati Kuu na ninarudia tena leo Chadema haijawahi kuteua wabunge wa viti maalumu” amesema Mbowe
Ещё видео!