Mkuu wa majeshi ya Kenya, jenerali Robert Kibochi amekosoa dhana kuwa serikali inajumuisha wanajeshi katika sekta ya utumishi wa umma. Hata hivyo, jenerali Kibochi amekariri kuwa jeshi limerejesha nidhamu na kuboresha utendakazi kwenye taasisi za umma zinazosimamiwa na maafisa wa kijeshi. Ameongezea kuwa mafanikio hayo yametokana na ustadi na kujitolea kwa jeshi katika kazi yake. Kibochi alidokeza kuwa jeshi la ulinzi la Kenya limesajili kampuni ya ujenzi ya Ulinzi ambayo itashiriki kwenye ujenzi wa barabara za kudumu kwa gharama nafuu kote nchini.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: [ Ссылка ]
Follow us on Twitter: [ Ссылка ]
Find us on Facebook: [ Ссылка ]
Check our website: [ Ссылка ]
#KBCchannel1 #KBCNews #Kenya
Ещё видео!