Tume ya uchaguzi imesisitiza kuwa itatumia mfumo wa kielektroniki kuwatambua wapiga kura siku ya uchaguzi. Kamishna wa IEBC Abdi Guliye akiwahutubiwa wanahabari alisema kuwa tayari shughuli ya kusambaza vifaa vya uchaguzi kote nchini ilikuwa imeanza na kuwa baadhi ya kaunti tayari zimepokea vifaa hivyo. Wakati huo huo tume hiyo imesema kuwa yeyote asiye kwenye sajili ya IEBC hatapata fursa ya kupiga kura.
Ещё видео!