Kuna namna mbili za akaunti za benk unazoweza penda kufungua.
Akaunti ya kutunza pesa au, akaunti ya akiba
Akaunti ya kutunza pesa, zinakupa uwezo wa kufikia pesa zako kwa urahisi ili uweze kutekeleza mahitaji yako ya kila siku.
Nayo Akaunti ya akiba inakuruhusu kuweka akiba kwa malengo ya muda mrefu, kama vile kununua gari au kusafiri.
Unaweza kupokea pesa kutoka akaunti ya hundi au, akaunti ya akiba kwa kutembelea benki yako. Unaweza kufikia pesa zako zilizomo kwenya akaunti yako na kuzitazama ukitumia kadi ya malipo kutoka kwa ATM au pia mara nyingine, unaweza kufikia akaunti yako ya akiba ukitumia kadi ya benki.
Tafadhali tazama video yetu kuhusu jinsi ya kutumia ATM.
Unaweza kufikia akaunti zote mbili kwenye kompyuta na simu yako.
Baadhi ya benki zina wafanya-kazi wenye ujuzi katika lugha mbalimbali, wakati mwingine zinakupa mkalimani kupitia kwa simu.
Jisikie huru kuuliza ikiwa benki yako inaweza kukuasaidia na mkalimani ikiwa utamuhitaji.
Unapoenda kufungua akaunti ya benki, benki itahitaji vitu fulani. Watahitaji jina lako, tarehe ya kuzaliwa, anwani, (ss) nambari ya usalama wa jamii na nambari ya simu ikiwa unayo.
Ikiwa wewe ni mkazi wa Marekani utahitaji kuonyesha benki vitu viwili kati ya hati hizi:
Pasipoti yako, Kadi yako ya Mgeni, Mkaaji au Mkazi wa Kudumu,
Kitambulisho chako cha Idara ya Jimbo la Marekani,
Visa yako ya Marekani au Kadi yako ya Uidhinishaji wa Ajira ya Marekani yenye Picha.
AU, unaweza kuwaonyesha mojawapo ya hati hizo, pamoja na Rekodi yako ya Kuwasili/Kuondoka ya I-94 au Leseni yako ya Udereva wa Kigeni.
Ikiwa wewe si mkazi wa Marekani utahitaji kuonyesha hati mbili kati ya hizi.
Pasipoti yako, Kadi yako ya Mkaaji Mgeni au Mkazi wa Kudumu
Idara yako ya Marekani. ya kitambulisho cha Jimbo
Visa ya Marekani, Kadi yako ya Uidhinishaji wa Ajira ya Marekani yenye Picha
AU Moja tu ya hati hizi, pamoja na Usajili wako wa Wapiga Kura kutoka serikali ya kigeni, Leseni ya Udereva ya Marekani au Nje, Cheti chako cha Kuzaliwa, Kitambulisho cha Picha cha Chuo, I-94 yako, au Visa ya Marekani iliyoidhinishwa.
Kisha, baada ya kukusanya nyaraka zote zinazohitajika, utahitaji kwenda kwenya benki na kumwomba usaidizi mfanyakazi aliye nyuma ya kaunta. Kumbuka kuulizia mkalimani ikiwa unamhitaji.
Unaweza kusema. “I would like to open a bank account” ambayo inamaanisha "Ningependa kufungua akaunti ya benki."
Mtu huyu anaweza kukusaidia kujua ni aina gani za Akaunti zinazotolewa katika Benki hiyo na ni akaunti gani ambayo inaweza kuwa bora kwako.
Unapofungua akaunti, benki nyingi zinahitaji uweke pesa. Mara nyingi kiaso hicho ni $25. Kwa hivyo tafadhali kumbuka kubeba $25 ili kufungua akaunti yako.
Benki tofauti zitakupa aina tofauti za akaunti walizo nazo . Ni muhimu kuelewa aina tofauti za akaunti ambazo zitakufaa wewe kulingana na kwa pesa ulizonazo.
Hapa kuna baadhi ya maswali ambayo unaweza kupenda kumuuliza mtu anayekusaidia.
Je, benki hutoza ada kwa kutunza pesa zangu na wao?
Je, kuna kiwango cha chini cha pesa ninacho paswa kuweka kwenye akaunti yangu bila kulipa ada yoyote?
Je, ni nini kitatokea ikiwa ninatumia pesa nyingi zaidi ya zile nilizo nazo kwenye akaunti yangu?
Je, ninaweza kupata pesa zangu ninapo safiri?
Watakuomba utie sahihi baadhi ya hati unapofungua akaunti ya benki. Hakikisha unaelewa kila hati kabla ya kuitia saini.
Unapofungua akaunti yako ya benki kuna uwezekano kwamba utapewa kadi ya malipo au itatumwa kwako kupitia njia ya barua.
Unaweza kupewa kitabu cha hundi pia. Cheki, ni hati iliyo-andikwa na ya tarehe inayo-iambia benki kulipa pesa kutoka kwa akaunti yako ya benk,i kwenda kwa mtu mwingine. Ni njia salama ya kutuma na kupokea pesa kupitia barua. Huenda ukahitaji hundi ili kulipa kodi au bili zako, au kutuma pesa kwa mtu ambaye anaishi mbali nawe.
Unafanya kazi kwa bidii ili kupokea pesa zako. Ni muhimu kujisikia vizuri na kurithika na benki ambayo itakuwa ikitunza pesa zako. Waulize marafiki zako au wanajamii kukushauri kuhusu benki ipi wapendayoi na, ni kwa nini. Kumbuka kuuliza mkalimani ikiwa unamhitaji.
Ещё видео!