"MUUNGANO SI WA WANASIASA NI MUUNGANO WA WANACHI TUWAACHIE WANANCHI WACHAGUE MUUNGANO WANAO UTAKA" Haya yalisemwa jana na Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh Yusuph Mwenda alipokuwa anafunga ziara ya Madiwani na watendaji toka Manispaa ya Zanziba ziara hiyo ya siku 5 ilikuwa na dhumini la kukuza urafiki na undugu uliopo kati ya Manispaa ya Kinondoni na Manispaa ya Zanzibar.Licha ya kuongea hayo Mstahiki Meya alikabidhi zawadi kwa wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano ya pasaka ambapo Timu ya madiwani Manispaa ya Kinondoni walipata kombe lililokabidhiwa kwa timu aptain Renatus Pamba na Timu ya watendaji wa manispaa ya kinondoni pia walipata kombe kwa hiyo makombe yote mawili yalibaki Kinondoni.
Ещё видео!