Mwenyekiti wa Taasisi ya Tunza Foundation Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum Mtwara mjini Tunza Malapo, amekabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi 40 kutoka shule 13 za sekondari za kutwa zilizopo Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Tunza Malapo amekabidhi vifaa hivyo ikiwemo Madaftari, kalamu,mashati ya shule na taulo za kike kwa wasichana leo Disemba 28, 2024 na kupata chakula cha pamoja na wanafunzi hao pamoja na wazazi wao, ikiwa ni ya shukrani kwa kutimiza mwaka mmoja tangu kuzinduliwa rasmi kwa taasisi hiyo.
Aidha Mwenyekiti huyo amesisitiza wazazi kusimamia vyema watoto wao kwa kushirikiana na Tunza Foundation, ili misaada inayotolewa iwe na tija na kutimiza malengo yake ya kuhakikisha watoto wanasoma kwa tabasamu.
"Vifaa hivi vinavyotolewa na taasisi yetu vitakuwa na maana kama watoto watasoma vyema na kutimiza malengo yao, pia wazazi hawanabudi kusisimamia vyema watoto ili tutimize malengo yao kwa pamoja" amesema Tunza Malapo.
Hata hivyo ameongeza kuwa Tunza Foundation Tanzania itaendelea kusadia watoto hao kwa kadri watakavyoendelea na masomo yao hadi chuo, hali ambayo itaongeza ari ya wanafunzi kusoma kwa bidii.
Taasisi ya Tunza Foundation Tanzania iliyoanza rasmi mwaka jana, tayari imesaidia wanafunzi takriban 80 ambao wapo kwenye mradi, na inatarajia kuendelea kuongeza wanafunzi wapya watakaoanza kidato cha kwanza mwaka 2025.
Ещё видео!