Wasimamizi wa vituo mbalimbali vya kufanyia mtihani kote Kisii wamehimizwa kuwa macho kila wakati ili kuzuia visa vya udanganyifu kwenye mtihani wa KCSE.
Akizungumza baada ya kufunguliwa rasmi kwa kasha la mtihani Kisii, mkurugenzi wa elimu Kisii Central, Cyrus Juma, amesema maafisa wa polisi wako ange kukabili visa vyovyote kwenye mtihani wa kitaifa. Kaunti ya kisii ina jumla ya watahiniwa 34,852 na vituo vya mtihani 372 ikiwemo vituo viwili kwenye magereza
Ещё видео!