Je ulisikiliza muziki wa waimbaji mahiri wa reggae wakiwemo Bob Marley, Peter Tosh, Alpha Blondy na Lucky Dube tangu utotoni mwako?
Leo kwenye #VijanaMubashara #77Asilimia tunaangazia historia ya muziki wa reggae ili kujua ni kwa nini wasanii wake, mistari na muziki wenyewe ungali maarufu hadi leo hususan barani Afrika.
Lakini pia tunasema makiwa kwa wapenzi wa reggae wanaomboleza kifo cha nguli wa aina hiyo ya muziki kutoka Jamaica Bunny Wailer aliyeaga dunia Machi 2, 2021 akiwa na umri wa miaka 73. Kabla ya kifo chake, Wailer aliyeanzisha kundi la the Wailers, ndiye msanii pekee aliyesalia miongoni mwa walioimba pamoja na Bob Marley na Peter Tosh.
Ещё видео!