Tunayo stori kutokea Jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya ambapo linawashikilia watu watatu wakiwemo raia wawili wa Nigeria pamoja na mwingine aliyejitambulisha kama Mchungaji kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya Dawa za Kulevya.
Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya Polisi Tanzania, ACP Alhaj Salim Kabaleke amesema Aprili 17, 2019 uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere walimkamata mtuhumiwa Linda Mazule raia wa Lativia akiwa na dawa za kulevya aina ya Heroin.
Amesema kutokana na hatua hiyo, Jeshi la Polisi lilifanya oparesheni jijini Dar es Salaam ambapo Aprili 21, 2019 waliweza kuwakamata watuhumiwa wengine watatu ambao ni Martins Plavin (20) raia wa Lativia, Henry Ugwuanyi (44) Mchungaji na Onyebuchi Ogbu (34).
Ещё видео!