"YESU anatajwa kama jiwe lililokataliwa na waashi yaani Israel na kuwa msingi wa mataifa waliompokea."
(Mdo 4:11-12, Efes 2:20-22)
YESU JIWE KUU, kwake wokovu wetu unakamilishwa maana hakuna jina jingine tulilopewa ambalo kwalo tunaokolewa isipokuwa jina lake.
* Jina lake linapita majina ya wakuu wote wa dunia hii na hakika ametukuka sana.
NOTE:
* Alikubali kubeba msalaba wa aibu, hakuona dhambi na maovu yetu kuwa kitu akatupenda tulivyo na kutuokoa.
* Alikubali mateso na kutoa uhai wake kwa kumwaga damu msalabani ili atupate sisi.
"Unaweza ukampa nafasi ya kuwa JIWE KUU LA MAISHA YAKO LEO kwa kumkubali moyoni mwako awe BWANA NA MWOKOZI KWAKO!!"
* Hatuna cha kumlipa zaidi ya kumwabudu na kuyatoa maisha yetu kama dhabihu iliyo hai kwake.....!!
Ungana nasi tumwambie YESU JIWE KUU NINAKUABUDU....!!!
Mdo 4:11-12
[11]Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.
[12]Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Waefeso 2:20-22
[20]Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
[21]Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.
[22]Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.
Ещё видео!