Mbunge Jimbo la Makete Mhe. Festo Sanga amewasihi wananchi kutunza na kulinda vyanzo vya maji kwa kila namna ili kuhakikisha vyanzo hivyo vinakuwa salama wakati wote.
Mhe. Sanga amesema hayo akiwa na wananchi wa Kitongoji cha Igofi Kijiji cha Kinyika Kata ya Kinyika Wilaya ya Makete kwenye Mkutano ambao alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi umuhimu wa vyanzo vya maji vinavyopatikana Makete na umuhimu wake kwa Taifa.
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Bw. Aloyce Malekela amesema watahakikisha vyanzo vya maji vinalindwa kwa kutofanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka chanzo cha maji ikiwemo kuwakamata wanaolima na kuchungia mifumo kwenye maeneo yaliyokatazwa.
Ещё видео!