Waziri wa Viwanda na Biashara Dk.Ashatu Kijaji ametoa wito kwa waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kuhakikisha bidhaa hizo zinakaguliwa ili kulinda afya za Watanzania, na wenye Viwanda vya ndani kuhakikisha bidhaa zinakaguliwa na Shirika la Viwango Tanzania(TBS) kabla ya matumizi.
Ametoa wito huo Septemba 18/09/2023 alipotembelea TBS kuona jinsi maabara za
TBS 4 kati ya 9, ikiwemo maabara ya chakula, ngozi, nguo na kemia
zinavofanya kazi na kusikiliza changamoto zilizopo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika Taasisi zote zilizopo chini ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023-2024 .
Aidha, Dk. Kijaji ameridhishwa na utendaji kazi wa TBS na kuitaka ifanye kazi kwa kushirikiana na Taasisi zingine ili kurahisisha utendaji kazi kwa kuhakikisha Watanzania wanatumia bidhaa bora na salama kwa afya zao.
Naye Kaimu Mkurugenzi Lazaro Msasalaga amesema TBS ina maabara tisa zenye vifaa vya kisasa, wataalamu wa kutosha na zina ithibati kimataifa inazozitumia kupima ubora na viwango vya bidhaa zinazozalishwa nchini na zinazoingia kutoka nje ya nchi.
Akitaja maabara hizo, Bw. Msasalaga amesema Maabara hizo ni Maabara ya Kemia, Maabara ya Uhandisi Ujenzi, Maabara ya Uhandisi Mitambo, Maabara ya Uhandisi Umeme, Maabara ya Kemia ya Chakula, Maabara ya Mikrobiolojia, Maabara ya Pamba, Nguo na Ngozi, Maabara ya Ugezi na Kituo cha Teknolojia ya Ufungashaji.
Follow us on:
FACEBOOK;
SpotiLeo: [ Ссылка ]...
HabariLeo: [ Ссылка ]
DailyNews: [ Ссылка ]
INSTAGRAM;
HabariLeo: [ Ссылка ]...
SpotiLeo: [ Ссылка ]...
TWITTER;
Twitter HabariLeo: [ Ссылка ]
Ещё видео!