Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu amewapongeza mamlaka ya maji dafi mkoa wa Dar es salaam na Pwani DAWASA kwakufanikisha kupeleka maji kwa wananchi wengi wa mikoa hiyo hali inayopelekea mpaka kugikia mwisho wa mwaka huu basi tatizo la maji litakua limeisha.
Hayo ameyasema wakati akikagua mradi wa maji wa kigamboni jijini Dar es Salaam ambao utasambaza maji katika jimbo la kigamboni na Mbagala na kufanikisha usambazaji maji katika mkoa mzima.
Makamu wa Rais amesema kwa wanayofanya DAWASA wasishangae watu kusikia mamlaka hiyo inaenda fanyakazi katika jiji la Dodoma kusaidia katika upatikanaji wa maji safi na salama kama Dar es salaam na kuipokesha serikali watalipwa baadae.
Ameongeza pia watu wanaofanya shughuli za kuuza maji katika wilaya ya kigamboni waache mala moja kusambaza maneno ya chuki kwa wananchi kua bili wanapewa kubwa zaidi tofauti na huduma wanayopewa jambo ambalo si kweli tofaut na gharama ambayo serikali imetumia ilikufikisha huduma kwa wananchi.
Ещё видео!