Zekaria 1:18 -21
Nami nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, pembe nne. Nami nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Nini hizi? Naye akanijibu, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, na Israeli, na Yerusalemu. Kisha BWANA akanionyesha wafua chuma wanne. Ndipo nikauliza Hawa wanakuja kufanya nini? Akasema kwamba, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, hata ikawa hakuna mtu aliyeinua kichwa chake; lakini hawa wamekuja kuzifukuza, kuziangusha pembe za mataifa, walioinua pembe yao juu ya nchi ya Yuda, ili kuwatawanya watu wake.
Katika Yuda hakuna mtu aliyekuwa anaweza kuinua kichwa chake( kukua &kuongezeka) kwa sababu ya zile pembe.
Hili jambo unaweza kuliona hata kwenye maisha ya kawaida. Kuna familia zinaweza kufika sehemu fulani (kimafanikio) lakini haziwezi kuvuka sehemu fulani.
Mtu atachukua mkopo, atapata ushauri mzuri lakini utakuta mwenzake aliyepewa ushauri kama wa kwake anafanikiwa lakini yeye hata ajitahidi vipi hawezi kufanikiwa.
Kwanini? - Kwasababu vita ya mwenzake sio kama vita yake. Mwenzake hakuna pembe iliyosimama kuhakikisha maisha yake hayaendi lakini yeye kuna pembe ambayo inahakikisha familia, ukoo wake HAUSOGEI.
Kabla hujaumia kuwa kwanini HAUSOGEI mbali na jitihada unazoweka tafuta kujua ni kwanini/nini kinakuzuia kusogea.
#PastorSunbella Kyando#Vifungo#Familia
Ещё видео!