Akizungumza katika Hafla hiyo Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji (Mb) ambaye pia ndiye Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Mafunzo hayo Amesema,"Kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 hadi 2025 Sura ya kwanza Ibara ya tisa A "Tunahitaji kuimarisha Utendaji wa Serikali za Mitaa ili ziweze kutimiza wajibu wao kwa Wananchi wa maeneo husika, Huwezi kuimarisha Utendaji usipokuwa na Elimu sahihi kwa kile unachokitenda".
"Kusoma ni jambo la muhimu na la msingi katika kila siku unapoamka, ni muhimu tukaendelea kujifunza hata tunapotaka kuboresha utendeji wetu kwenye majukumu yetu Mbalimbali".Amesema Dkt.Ashatu.
Dkt.Ashatu Amesema kupitia Mafunzo haya ya Utawala Bora huduma kwa wananchi inakwenda kuboreka kutokana na yale ambayo Viongozi walikuwa hawayajui wayafanye vipi sasa wanakwenda kuyajua ni namna gani wayafanye kwa Wananchi hao.
Aidha,Dkt.Ashatu Amewataka Wananchi wa Kondoa kuwa tayari kwa Huduma iliyoboreka, kuwa tayari kuhudumiwa na Viongozi Weledi kutokana na pale ambapo kulikuwa na Mapungufu sasa yanakwenda kurekebishwa hivyo wajiandae kupokea Huduma iliyoboreshwa.
#millard #ikulu #eatv #itv #onestepmediatz #tbc #clips #cloudsfm #mwanachidigital
Ещё видео!