UFUGAJI WA NGURUWE KIBIASHARA
Nguruwe ni mnyama anaefugwa kwajili ya kitoweo na nyama yake ni nyeupe (White meat).
Nguruwe ni mnyama ambae anauwezo wa kuzaa mtoto zaidi ya mmoja (multiparous) na ni kati ya wanyama wanao nyonyesha (mamaria).
Nguruwe ni mnyama anaekula vyakula vya aina tofauti kama ilivyo kwa binadamu, yaani yupo kwenye group la Omnivorous (feed varieties)
Ufugaji wa nguruwe unaendelea kukuwa kwa kasi sana hapa Tanzania na Africa mashariki, ni kati ya ufugaji unaofanyika KIBIASHARA kwa lengo la kuingiza kipato.
Miaka ya hivi karibuni Tanzania tumefanikiwa kuingiza mbegu bora za kisasa za nguruwe zenye uwezo wa kukuwa ndani ya muda mfupi tofauti na mbegu za kienyeji.
Nguruwe mmoja anauwezo wa kuzaa watoto 10 na zaidi, na ndani ya mwaka huzaa mara 2.
Watoto wa nguruwe wa kisasa ukiwatunza vizuri unaweza wauza kama nyama ndani ya siku 90.
Nguruwe wa kisasa wanauwezo wa kufikisha uzito wa kilo 35 hadi 45 ndani ya miezi 3, tangu kuzaliwa, tofauti na nguruwe wa kiswahili.
Kwa ukuaji huu wa haraka, biashara ya ufugaji wa nguruwe imekuwa yenye faida sana, ingawa changamoto kubwa kwa sasa ni gharama za vyakula zipo juu.
Gharama za chakula kwenye ufugaji wa nguruwe huchukua asilimia 70 ya gharama za uendeshaji.
Endelea kuwa nasi JOACK Company LTD ili uweze kujifunza zaidi mambo ya msingi yanayohusina na ufugaji KIBIASHARA.
JOACK tunatoa ushauri kwa njia ya simu, kufika ofisini au kwa kukutembelea shambani/site kwako.
Karibu sana......
#nguruwe #nguruwewakisasa #ufugajiwanguruwe #nyama #nyamayanguruwe #watotowanguruwe #nguruwebora #mbeguzanguruwe #pig #pigfarming #pigfarmingintanzania #wafugajiwanguruwe #chakulachanguruwe #nguruwewazazi #wauzajiwanguruwe #vifaavyanguruwe #madumeyanguruwe #upandishajiwanguruwe
Office zetu zipo @tegetawazohill Barabara ya kwenda kiwanda cha twigacement, opposite na kota za kiwanda - Dar es salaam, Kwa wanaohitaji bidhaa zetu au huduma yoyote fika ofisini au wasilina nasi kwa
Simu:
+255 655 05 73 23 (WhatsApp)
+255 692 43 02 63
Email:
joackbagamoyo@gmail.com
#joackcompany #mifugo #kilimo #kilimotz #mifugotz #mabandayamifugo #mabanda #ujenziwamabanda #dodoma #tanzania🇹🇿 #tanzania #mwanza
JOACK COMPANY LTD
Ещё видео!