Mkazi wa Tabata, Jijini Dar es Salaam, Mwasema Rashid anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Iringa kwa tuhuma za kukutwa na kete 58 za dawa za kulevya.
Rashid anayedaiwa kuwa alikuwa safarini akitokea Msumbiji kuingia nchini Tanzania kwa kupitia barabarara ya Mbeya – Dar es Salaam alibanwa na tumbo kisha kwenda kutibiwa katika zahanati ya Mtandika, Wilayani Kilolo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Allan Bukumbi amewaambia waandishi wa habari kuwa kutokana na maumivu ya tumbo akiwa kwa daktari alilazimika kueleza ukweli kuwa alimeza pipi za dawa za kulevya.
"Hadi sasa mtuhumiwa ameshatoa pipi 58 kupitia njia ya haja kubwa chini ya uangalizi wa Madaktari na polisi,” amesema Bukumbi.
#Iringa
#madawa #polisi #iringa
Ещё видео!