KHAMIS MADATA MGEJA ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga amejitosa tena kuwania tena nafasi hiyo ambapo amekabidhiwa rasmi fomu za kugombea na Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Daudi Magessa.
Mgeja amesema amechukua uamuzi wa kuwania nafasi hiyo muhimu ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya mkoa ikiwa ni haki yake ya kikatiba kama mwanachama wa CCM aliyetimiza sifa za kugombea.
"Nimeona kwamba ninao uwezo wa kuongoza, lakini kikubwa zaidi ni kuviachia vikao vya chama ndivyo vitakavyoamua, kwa leo sintakuwa na mengi ya kuzungumza kwa siku ya leo lakini itoshe tu kufahamu kwamba nimetumia haki yangu ya kikatiba kama mwanachama wa CCM kuchukua fomu ya kuomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa," anaeleza Mgeja.
Ещё видео!