Rais Samia Suluhu Hassani amesema wameamua kutafuta fedha kwa wadau mbalimbali ili kuiinua sekta ya kilimo kutokana na hali ilivyo sasa ya tishio la uhaba wa chakula katika mataifa mengine iliyosababishwa na mabadiliko ya Tabianchi.
Ameyasema hayo wakati akizindua Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) kwa mwaka 2023 pamoja na Baraza la Kuangalia Utoshelevu wa Chakula Tanzania.
Ещё видео!