Simba SC imeishushia kichapo kizito cha mabao 5-0 Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.
Pape Ousmane Sakho amefunga magoli mawili dakika ya 48 na 90 huku mengine yakitoka kwa Mzamiru Yassin dakika ya 38, Augustine Okrah dakika ya 63 na Moses Phiri dakika ya 73.
Katika mchezo huo pia, wachezaji wawili wa Mtibwa Sugar Pascal Kitenge na Cassian Ponera walitolewa kwa kadi nyekundu kwa mchezo usiokuwa wa kiungwana.
Ещё видео!