ZAB 124
Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,
Israeli na aseme sasa,
Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,
Wanadamu walipotushambulia.
Papo hapo wangalitumeza hai,
Hasira yao ilipowaka juu yetu
Papo hapo maji yangalitugharikisha,
Mto ungalipita juu ya roho zetu;
Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu
Maji yafurikayo.
Na ahimidiwe BWANA;
Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.
Nafsi yetu imeokoka kama ndege
Katika mtego wa wawindaji,
Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.
Msaada wetu u katika jina la BWANA,
Aliyezifanya mbingu na nchi
Maarifa ya Ki-Mungu
@SIRI ZA BIBLIA
www.sirizabiblia.com
+255 758 708 804
[ Ссылка ]
Instagram Account
[ Ссылка ]
SADAKA YAKO YA KUCHANGIA INJILI IFIKE MBALI ZAIDI:
M-PESA +255 758 708804 INNOCENT MASHAURI
CRDB ACC: 0152523574100 INNOCENT LEONARD MASHAURI
Ещё видео!