Zaburi 121, Kiswahili
Mungu kinga yetu
1 Natazama juu milimani;
msaada wangu utatoka wapi?
2 Msaada wangu watoka kwa Mungu,
aliyeumba mbingu na dunia.
3 Hatakuacha uanguke;
mlinzi wako hasinzii.
4 Kweli mlinzi wa Israeli
hasinzii wala halali.
5 Mungu ni mlinzi wako;
yuko upande wako wa kulia kukukinga.
6 Mchana jua halitakuumiza,
wala mwezi wakati wa usiku.
7 Mungu atakukinga na baya lolote;
atayalinda salama maisha yako.
8 Mungu atakulinda katika shughuli zako zote
tangu sasa na hata milele.
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa
Ещё видео!