Polisi wamerusha vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakipinga mswada tata wa fedha wa mwaka 2023 katikati mwa jiji la Nairobi. Waandamanaji hao walikongamana katika Bustani la Jivanjee kuandamana, kabla ya kuanza safari kuelekea majengo ya bunge. Hata hivyo waandamanaji hao waliokuwa wamebaba mabango ya kupinga mswada huo walifurushwa na maafisa wa usalama walioshika doria. Waandamanaji kadhaa wamekamatwa wakawa maandamano hayo. Kumekuwa na pingamizi kuhusu mswada huo huku serikali ikishikilia kuwa ni lazima utaidhinishwa na bunge
Ещё видео!