Washika dau katika sekta ya elimu eneo la Kiharu, kaunti ya Murang'a, wameshinikiza wanafunzi wa gredi ya 6, 7 na 8 wasalie katika shule za msingi. Wakizungumza wakati wa maombi kwa matayarisho ya mtihani wa gredi ya 6 na darasa la 8 KCPE katika shule ya msingi ya St Martin, wasimamizi na wazazi wa shule hiyo wamesema shule nyingi za msingi zina uwezo wa kuwahudumia wanafunzi hao na madarasa ya kutosha ikilinganishwa na shule za sekondari. Baadhi ya wazazi pia wameonekena kukumbatia mfumo wa CBC wakisema watoto wao wanaendelea kupata elimu itakayowasaidia kujisimamia maishani
Ещё видео!