Miaka 25 sasa bila ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye historia ya Tanzania haiwezi kulikana jina lake kama ilivyo kwenye historia ya Chama Cha Mapinduzi CCM huku pia sisi Arusha tukiwa na kurasa zetu kadhaa katika historia ya siasa za Tanzania - Azimio la Arusha ambalo pia lilisimamiwa na kuasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere.
Kwenye picha tano za harakati za Mwalimu Nyerere huwezi kukosa Gari chapa ya Land Rover; Hizi ndizo gari zilizotumika kwenye harakati za kuudai uhuru wa Iliyokuwa Tanganyika, Hii ndiyo gari iliyotumika kwenye mapambano ya kukikuza Chama cha TANU na ASP mpaka baadae ilipokuja kuzaliwa CCM na hata itikadi na falsasa za Azimio za Arusha zilitangazwa na kutekelezwa kona zote za nchi kwa kutumia usafiri chapa ya Land Rover.
Kwa waliojaliwa uwezo wa kununua magari pia miaka hiyo, usafiri uliokuwa si tu ukiendana na barabara za wakati huo bali pia "Usasa" wa wakati huo, bhasi gari chapa ya Land Rover ilikuwa ni aghalabu kuikana ama kuikataa sokoni.
Wakati huu tunapoelekea kwenye Rekodi mpya ya dunia kupitia Land Rover Festival 2024 inayofanyika kuanzia Oktoba 12-14, 2024 Jijini Arusha, bhasi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda anatukumbusha kuwa zipo sababu zaidi ya elfu moja ambazo zinatufanya sote wana familia ya Land Rover tujumuike pamoja kusherehekea na kuweka historia na rekodi isiyomithilika tukiwa kwenye Land Rover zetu bila kujalisha ni ya kizazi gani.
Ещё видео!