Zaburi 142- SALA
1. Kwa sauti yangu nitamlilia Bwana, Kwa sauti yangu nitamwomba Bwana dua.
2. Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake.
3. Nilipozimia roho uliyajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego.
4. Utazame mkono wa kuume ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho.
5. Bwana, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai.
6. Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye nao wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.
7. Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikarimu.
Ещё видео!