Samson Ryoba mgombea udiwani kata ya Kisangura jimbo la Serengeti amesema akiwa Chadema alipata upinzani mkubwa katika kutekeleza ahadi zake kwa wananchi katika kipindi cha mwaka 2015-2020. Mgombea huyo aliyehamia CCM katika uzinduzi wa kampeini zake amesema alijitahidi kutekeleza miradi mbalimbali ya elimu na afya ikiwemo ujenzi wa lambo la mifugo na wananchi na kuwaomba wananchi wamumpigie kura kwa kuwa sasa yuko CCM itakuwa rahisi kutimiza ahadi zake.
Ещё видео!