Yanga SC wametupwa nje ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2020 kwa penati 4-2 na Mtibwa Sugar baada ya sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo wa nusu fainali uliopigwa kwenye Dimba la Amaan Zanzibar.
Bao la Kibwana Shomary dakika ya 90+2 likiisawazishia Mtibwa ndilo lililoupeleka mchezo huo kwente matuta baada ya Yanga kutangulia kupata bao dakika ya 37 kupitia kwa Deus Kaseke.
Mtibwa wamefunga penati nne, ya mwisho ikifungwa na yule yule Kibwana Shomary huku penati ya Abdulhalim Humud ikidakwa na golikpa Ramadhan Kabwili wakati Yanga wakipata penati mbili na kukosa mbili kupitia kwa Kelvin Yondan na Abdulaziz Makame, waliofunga wakiwa Paul Godfrey na Mapinduzi Balama.
Ещё видео!