Simba imelazimisha sare ya bao 1-1 mbele ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya #AfricanFootballLeague uliopigwa kwenye Dimba la Cairo nchini Misri.
Simba wametangulia kwa goli la Sadio Kanoute dakika ya 68 kabla ya Ahly kuchomoa kwa goli la Mahamoud Kahraba dakika ya 75.
Matokeo haya yanaisukuma nje Simba kwa hasara ya goli la ugenini kufutia sare ya 2-2 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Jijini Dar es Salaam.
Ещё видео!