Dalili za Mimba ya Mapacha huwa ni sawa kabisa na Dalili za Mimba ya Kawaida Ispokuwa tuu wakati mwingine,Dalili za Mimba ya Mapacha huwa zaidi kuliko Mimba ya kawaida na hii wanaoweza kujingundua ni akina Mama ambao wanauzoefu kwa maana kwamba wale ambao walishakuwa na mimba Mara kadhaa siku za nyuma na wakajifungua.
Endapo Mama anapata Mimba kwa Mara ya kwanza siyo rahisi kuweza kujigundua kuwa ana mimba mapacha.
Dalili hizo huweza kuwa kama hizi zifuatazo.
1. Kutapika au kuona kichefu chefu asubuhi (Morning Sickness) huwa ni zaidi ukilinganisha na wale wenye mimba ya kawaida.
Kumbuka kama Mama mjamzito ni Mara ya kwanza kuwa mjamzito au mimba ya kwanza au hata kwa wengine kuna magonjwa mengine mfano kutapika wakati wa ujazito (Hyperemesis Gravidarum) huwa na Dalili hizo pia
2. Kuchoka mara kwa mara na zaidi hii ni kutokana na mabadiliko ya kimwili na homoni za mwanamke wakati wa ujauzito lakini pia kwa sababu ya uzito mkubwa wa watoto wawili.
3. Kuanzi wiki ya 16 Mama ambaye aliwahi kuwa na mimba miaka ya nyuma ataona watoto wanacheza mara nyingi zaidi kuliko kawaida.
4. Kuongezeka kwa uzito wa Mama kwa kasi zaidi na kuwa na uzito mkubwa kuliko Mama mwenye Mimba ya kawaida, kwa kawaida uzito huongezeka kwa wastani wa (11-25)kg kwa kipindi chote cha mimba kwa akina mama wenye uzito wa kawaida wanapokuwa na ujauzito hivyo basi,
Kumbuka magonjwa ya shinikizo kubwa la damu (Gestational hypertension, Preeclampsia na Eclampsia) huweza kuwa na Dalili hii za kuongezeka kwa uzito mkubwa hivyo ukifikisha miezi mitano hakikisha unajua presha yako na ujiridhishe kuwa ni ya kawaida.
5. Tumbo kuongezeka ukubwa kuliko umri wa mimba,hii ni kwa sababu ya uwepo wa watoto wawili tumboni,kumbuka siyo Mara zote tumbo la mama mjamzito kuongezeka kwa kasi zaidi kuliko kawaida ina maanisha kuwa mimba ya mapacha wakati mwingine huwa kuna magonjwa(Gestational Trophoblastic Diseases,Polyhydromnios/Hydromnios) ambayo huweza kuwa na Dalili hii pia kwa hiyo usijichanganye.
NB;Ukiwa unaswali unaweza kuuliza hapa chini (kwenye comments za youtube).
©Dr.Mwanyika.
#AfyaBora
#JapideAfya_Services
#DaliliZaMimbaYaMapacha
Ещё видео!