"HAKUNA UHABA WA SUKARI NCHINI" - WAZIRI HASUNGA AKAGUA MAGHALA, ATOA MAAGIZO MAZITO...
Serikali imetangaza kuendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara nchini wanaotumia uwepo wa ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID 19) kuhodhi kiasi cha sukari kinachokuwa kwenye mzunguko na kuuza kwa bei ya juu zaidi ya bei ya ukomo katika eneo husika ambayo ni kati ya Shilingi 2600 hadi 3200.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 16 Mei 2020 wakati akifanya ziara ya kushtukiza Jijini Dar es salaam ili kukagua na kujionea hali ya upatikanaji wa sukari nchini.
Mhe Hasunga amesema kuwa serikali imeweka mbinu kali za kuwabaini wafanyabiashara hao na punde watakapobainika watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria za nchi.
Ametangaza hali ya upatikanaji wa sukari nchini kuwa imeendelea kuimarika ambapo kufikia tarehe 16 Mei 2020 kiasi cha Tani 18,142 kimeingia nchini kati ya kiasi cha Tani 40,000 kilichoagizwa na wazalishaji wa ndani kwa ajili ya kuziba pengo la uzalishaji wa msimu wa mwaka 2019/2020.
Amesema kati ya kiasi hicho cha Tani 18,142 kilichoingizwa kiasi cha Tani 15,498 kimetolewa bandarini na mipakani na tayari kipo sokoni na kingine cha Tani 2,644 kipo katika hatua mbalimbali za kutolewa bandarini.
Amebainisha kuwa tarehe 16-22 Mei 2020 zitaingia Tani 7470, Tarehe 23-31 Mei 2020 zitaingia Tani 13,404, huku tarehe 1-4 Mei 2020 kiasi cha Tani 984 kitawasili nchini.
Kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali kukabiliana na upandaji holela wa bei, Waziri Hasunga amesema kuwa serikali ilitoa bei elekezi kupitia GN Na 284 na 352 ya tarehe 24 Aprili 2020 na tarehe 8 Mei 2020 mtawalia, na kufanya msako wa wafanyabiashara wasio waadilifu wanaouza sukari kinyume na bei elekezi kwa kushirikiana na mamlaka zingine za kiserikali.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:[ Ссылка ]
⚫️ iOS:[ Ссылка ]
⚫️ VISIT AMAZON: [ Ссылка ]
⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE ( +255 784 888982), ( +255 713 837506)
⚫️ Email: globaltvbest@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com
⚫️ OUR PLAYLISTS:
⚫️ HABARI MPYA DAILY:shorturl.at/mnux2
⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: [ Ссылка ]
⚫️ GLOBAL RADIO TV: [ Ссылка ]
⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: [ Ссылка ]
⚫️ Subscribe Global TV [ Ссылка ]
Ещё видео!