179 SIKU moja mavuno yataisha kabisa
Nyimbo Za Wokovu
#Nyimbozawokovu
1. Siku moja mavuno yataisha kabisa,
baada ya hayo hukumu.
Jua litazimika siku hiyo ya mwisho,
na hutasikia injili
Refrain:
Atakusanya ngano kwa furaha ghalani
bali makapi yote yatatupwa motoni
rafiki utakuwa wapi
2. Mahubiri na nyimbo za wokovu wa mungu
zitakaponyamaza huku,
uliyelikataa neno zuri la mungu,
utakaa wapi milele
3. Watu wote wa mungu wafikapo mbinguni
kukaa pamoja na yesu,
wataimba kabisa kwa sauti nguvu
kumshangilia mwokozi
Ещё видео!